Tanzania's national professional home for business development service providers; setting standards, building capacity, powering enterprise growth.

Search BDS Tanzania
Contact Information
Location Dodoma, Tanzania
Follow BDS Tanzania
Contact Information
Location Dodoma, Tanzania
Follow BDS Tanzania

BDS TANZANIA YAPELEKA HUDUMA ZA USHAURI WA BIASHARA SABASABA

Back to Updates
BDS TANZANIA YAPELEKA HUDUMA ZA USHAURI WA BIASHARA SABASABA

BDS TANZANIA YAPELEKA HUDUMA ZA USHAURI WA BIASHARA SABASABA

Business Development Society of Tanzania (BDS Tanzania) ilitumia Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kujitambulisha kwa umma na kuonesha kwa vitendo nafasi ya wataalamu wa maendeleo ya biashara katika kukuza biashara ndogo na za kati. Kupitia kliniki za biashara, wataalamu wa BDS Tanzania walitoa ushauri kuhusu urasimishaji, uzingatiaji wa sheria, utunzaji wa kumbukumbu za fedha, maandalizi ya mipango ya biashara, upatikanaji wa mitaji na kuunganisha wafanyabiashara na taasisi husika. Mchumi Mwandamizi wa NEEC, Ndg. Berry Yongolo, alieleza kuwa Sabasaba ni jukwaa muhimu la kuwasaidia wananchi kufahamu fursa za uwezeshaji, kupata taarifa sahihi na kuelewa namna ya kushiriki katika programu mbalimbali. Alibainisha pia kuwa ushirikiano na taasisi kama BDS Tanzania unaongeza wigo wa elimu na ushauri unaotolewa kwa wafanyabiashara. NEEC pia ilisaidia kuwaunganisha washiriki na taasisi zinazohusika na usajili wa biashara, kodi, viwango vya bidhaa, uwekezaji na maendeleo ya viwanda vidogo. Hatua hiyo ilipunguza changamoto ya wajasiriamali kutofahamu taasisi sahihi ya kwenda wanapohitaji huduma maalumu. Ushiriki wa NEEC katika Sabasaba umeonesha umuhimu wa taasisi za umma kutosubiri wananchi wazifuate ofisini pekee, bali kupeleka huduma na taarifa katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya wajasiriamali. Kupitia maonesho hayo, Baraza liliweza kusikiliza changamoto, kutoa mwongozo na kuimarisha uelewa wa umma kuhusu uwezeshaji wa kiuchumi.
Share this update:

More Updates

View All Updates